Meli ya kwanza inayotumia upepo duniani inatarajiwa kuanza safari yake ya majaribio siku ya Ijumaa
Meli ya kwanza inayotumia upepo duniani inatarajiwa kuanza safari yake ya majaribio siku ya Ijumaa ikitokea Antwerp nchini Ubelgiji.
Chombo hicho chenye uzito wa tani 16,000 maarufu kama ‘The MT Chemical Challenger’ ni sehemu ya majaribio ya uwezo wake wa kuelea majini kwa kutumia nishati ya upepo pekee.
Kulingana na muongozo uliotolewa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Baharini, uzalishaji wa hewa chafu kutoka kwenye vyombo vya majini unatakiwa kupungua kwa asilimia 40 ifikapo 2030 kulingana na makubaliano ya Paris yaliyofikiwa mwaka 2015.
Share: