Mauzo ya simu aina ya iphones yameshuka katika masoko ya kimataifa

Kampuni hiyo ilisema takwimu hizo zilipotoshwa na usumbufu wa usambazaji unaohusiana na Covid

Mauzo ya simu aina ya iPhones yameshuka katika karibia masoko yote ulimwenguni, kulingana na matokeo ya hivi punde kutoka Apple.

Kampuni hiyo kubwa ya teknolojia ilisema mahitaji ya jumla ya simu zake mahiri yamepungua kwa zaidi ya 10% katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu, huku mauzo yakishuka katika kila eneo la kijiografia isipokuwa Ulaya.

Apple ilisema kuwa kwa ujumla, mapato katika kampuni yote yalipungua kwa 4% hadi $90.8bn (£72.5bn), ambayo ilikuwa kushuka kukubwa zaidi kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Hatahivyo, matokeo hayakuwa mabaya kama ilivyotarajiwa na bei ya hisa ya Apple ilipanda katika biashara ya saa baada ya saa huko New York.

Kampuni hiyo ilisema takwimu hizo zilipotoshwa na usumbufu wa usambazaji unaohusiana na Covid, ambao ulisababisha mauzo yenye nguvu isiyo ya kawaida katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Iliahidi kwamba mauzo yangerejea katika ukuaji katika miezi ijayo, ikibainisha uzinduzi ujao wa bidhaa na uwekezaji katika akili mnemba (AI).

Kwa iPhone, mauzo katika soko kuu la China yalipungua kwa 8%. Bw Cook alijaribu kuwahakikishia wawekezaji kuhusu hali ya biashara katika uchumi wa pili kwa ukubwa duniani, akibainisha kuwa mauzo ya iPhone yalikuwa yameongezeka nchini China.







Share: