Mamlaka ya saudia imeruhusu matumizi ya nguvu kupita kiasi kuwafurusha raia kwa ajili ya mradi wa mji wa neom

Mamlaka ya Saudia imeruhusu matumizi ya nguvu kupita kiasi kuwafurusha raia kwa ajili ya mradi wa mji wa jangwani wa siku zijazo unaojengwa na makumi ya makampuni ya Magharibi, afisa wa zamani wa ujasusi ameiambia BBC.

Kanali Rabih Alenezi anasema aliamriwa kuwafurusha wanakijiji kutoka kabila moja katika jimbo la Ghuba ili kutoa nafasi kwa ‘The Line’, sehemu ya mradi wa mazingira wa eneo la Neom.

Mmoja wao alipigwa risasi na kuuawa kwa kupinga kufurushwa kwake, Serikali ya Saudia na usimamizi wa eneo la Neom walikataa kutoa maoni.

Neom, eneo la ekolojia la Saudi Arabia la $500bn (£399bn), ni sehemu ya mkakati wake wa Saudi Vision 2030 ambao unalenga kuleta mseto wa uchumi wa ufalme huo mbali na mafuta.

Kampuni nyingi za kimataifa, zikiwemo za Uingereza, zinahusika katika ujenzi wa eneo la Neom.

Eneo hilo ambalo linajengwa limefafanuliwa kama "turubai tupu" na kiongozi wa Saudi Mrithi wa Kifalme Mohamed bin Salman. Lakini zaidi ya watu 6,000 wamehamishwa kwa ajili ya mradi huo kulingana na serikali yake - na shirika la haki za binadamu lenye makao yake nchini Uingereza ALQST linakadiria kuwa idadi hiyo ni kubwa zaidi.

Picha za satelaiti za vijiji vitatu vilivyobomolewa - al-Khuraybah, Sharma na Gayal. Nyumba, shule na hospitali zimefutwa kabisa kwenye ramani.









Share: