Kwenye ulimwengu wa biashara, makampuni kama Spotify, TikTok, na Uber yamepindua meza kwa kuunda majukwaa yanayofanikiwa bila kumiliki rasilimali yoyote zaidi ya program za simu.
Yafuatayo ni mifano ya makampuni yaliyofanikiwa kwa mtindo huu:
1. Spotify: Ina thamani ya dola bilioni 15 bila kumiliki hata kipande cha muziki, ikitegemea wasanii na rekodi zao.
2. YouTube: Imefikia thamani ya dola bilioni 31 bila kumiliki video zinazopakiwa na watumiaji.
3. Airbnb: Jukwaa hili la malazi lina thamani ya dola bilioni 9 bila kumiliki hoteli hata moja.
4. Doordash: Ina thamani ya dola bilioni 8, ikihusisha migahawa bila kumiliki hata mmoja.
5. Uber: Kampuni ya usafiri yenye utajiri wa thamani ya dola bilioni 37 bila kumiliki magari.
6. Instagram: Ina thamani ya dola bilioni 49 bila kutengeneza maudhui yake kama ilivyo kwa watumiaji wake, amabo hulipwa kwa kuunda maudhui.
7. TikTok: Ina thamani ya dola bilioni 16 huku ikitegemea video zinazotengenezwa na watumiaji wake.
Makampuni haya yameonyesha jinsi ujasiriamali wa kidigitali unavyoweza kuunda thamani ya pesa kubwa kupitia teknolojia na ugunduzi wa majukwaa. Je, una wazo la kuunda jukwaa kama hili? Inawezekana, na mifano hii ni ushahidi tosha.