Makampuni mbalimbali ya usafirishaji ulimwenguni yakumbwa na hitilafu ya kiteknolojia

Biashara mbalimbali duniani zikiwemo Benki,usafiri wa anga, Matreni, Makampuni ya teknolojia ya habari zimekumbwa na hitilafu kubwa ya kiteknolojia.

Hitilafu hiyo imesababisha matatizo makubwa ikiwemo kusimama kwa huduma za usafiri na kukwama kwa upasuaji kadhaa mahospitalini.

Mashirika makubwa ya Ndege kama American Airlines, Delta Airlines na yamesimamisha baadhi ya safari zake huku viwanja vya ndege kadhaa vya Ujerumani, Uhispania na Amsterdam vikiripoti hitilafu.

Kuharibika kwa teknolojia ya habari (IT) hakuhusiani na shambulio la kimtandao.

Makampuni husika yanafanya juhudi za kila namna na za haraka ili kuweza kurudisha hali ya kawaida.

Share: