Jkci yavunja rekodi matibabu ya moyo

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu alisema uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika sekta ya afya hii ikiwa ni pamoja na kujenga majengo ya kisasa, kusomesha wataalamu na kuunua vifaa tiba vya kisasa kumewezesha kufanyika kwa upasuaji huo.

Dk Jingu alisema kutokana na umuhimu mkubwa wa sekta ya afya Serikali itaendelea kuboresha huduma ya afya ikiwa ni pamoja na kusomesha wataalamu katika nchi mbalimbali ambao watakuja kutoa matibabu ya kibingwa nchini.

Kwa Julai hadi Desemba mwaka huu alidokeza kuwa JKCI imehudumia zaidi ya wagonjwa 3,000 katika kufanya upasuaji mkubwa na mdogo wa moyo na kusisitiza Serikali itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kibingwa za matibabu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge aliishukuru Serikali kwa kuiwezesha Taasisi hiyo ambayo imeweza kufanya matibabu hayo ya kihistoria ambapo kwa nchi za Afrika hakuna hospitali ya Serikali inayotoa huduma hiyo.

Share: