Infinix yazindua toleo la note 40 nchini malaysia

Unaambiwa Wapenzi wa game hata waliopo Tanzania kupitia infinix mobile tz wamefikiwa kwa ukaribu kwa sababu NOTE 40 ina 7020 na chipsets za Helio G99 Ultimate zenye hadi RAM ya 24GB

Kampuni ya simu za mkononi Infinix leo hii imezindua rasmi simu mpya za toleo la NOTE 40 katika Circuit maarufu ya Kimataifa inayofahamika kama F1 Depang nchini Malaysia.

Uzinduzi huu unaoshiria mapinduzi makubwa ya teknolojia ya Fast Charge, ulitanguliwa na Infinix kuonyesha Maabara yake ya ‘All-Round Hyper Speed ambapo sifa kubwa kwa toleo hilo la NOTE 40, NOTE 40 pro, NOTE 40 Pro 5G na NOTE 40 Pro+ 5G ni teknolojia bunifu ya All Round FastCharge 2.0 inayosaidia 100W Multi-Speed FastCharge, Wireless MagCharge na Chip Infinix iliyojitengenzea Cheetah X1’inayofuatilia hali nzima ya kuchaji.

NOTE 40 Pro+ 5G inajivunia 100W Multi-Speed FastCharge, inakupa 50% ndani ya dakika 8 kwa kutumia teknolojia ya hypermode lakini pia katika kuendana na hali ya kimazingira ya simu, hali ya hewa Mtumiaji anaweza tumia low temp mode au smart mode kwani nguvu kubwa imewekwa katika battery inaweza kupokea mizunguko ya chaji kwa takribani mara 1600 na nguvu ya battery kuendelea kuwepo kwa asilimia 80%.

Unaambiwa Wapenzi wa game hata waliopo Tanzania kupitia infinix mobile tz wamefikiwa kwa ukaribu kwa sababu NOTE 40 ina 7020 na chipsets za Helio G99 Ultimate zenye hadi RAM ya 24GB, udhibiti wa kasi ya fremu ya XBOOST inayoboresha utendakazi wa michezo, huku spika mbili za stereo zinazotolewa na JBL zikitoa ubora wa sauti kamili.

Sifa yengine ni umbo la 3D lililopinda, 120Hz AMOLED na mfumo thabiti wa kamera wa 108MP wa kukuza zaidi ambapo usaidizi wa OIS katika Infinix NOTE 40 viboreshaji vya AI na Sauti by JBL kwa utendakazi usio na kifani.

Share: