Gavana wa florida amesaini muswada unaopiga marufuku watoto wenye umri chini ya miaka 14 kutumia mitandao ya kijamii

Gavana wa Florida, Ron DeSantis amesaini Muswada ambao unapiga marufuku Watoto wenye umri chini ya Miaka 14 kutumia Mitandao ya Kijamii na kuhitaji Watoto wenye umri wa Miaka 14 na 15 kupata idhini ya Wazazi, hatua ambayo inalenga kuwalinda na hatari za Mtandaoni kwenye Afya ya Akili

Muswada huo unazitaka Kampuni zinazomiliki majukwaa ya Mitandao ya Kijamii kusitisha akaunti za Watu wenye umri chini ya Miaka 14 na za wenye umri chini ya Miaka 16 ambao hawana idhini ya Wazazi

Baadhi ya Watu wanaamini Sheria hiyo itaondoa athari mbaya za Mitandao ya Kijamii kwa ustawi wa Watoto ambao wanatumia majukwaa hayo kwa wingi na wanaweza kupata wasiwasi, kunyongea na magonjwa mengine ya Akili

Share: