Ers-2 satelaiti ya zamani kuanguka saa chache zijazo tangu kumalizika kwa shughuli zake 2011

Satelaiti ya kwanza ya Ulaya inatarajiwa kuanguka duniani saa chache zijazo.

Lengo la ERS-2 ilikuwa kuchunguzi anga ilipozinduliwa mwaka wa 1995, na kuunda teknolojia ambazo sasa zinatumika mara kwa mara kufuatilia sayari.

Imekuwa ikishuka hatua kwa hatua tangu kumalizika kwa shughuli yake mwaka 2011 na itachukua mkondo usio na udhibiti na hatari katika angahewa siku ya Jumatano.

Shirika la Anga za Juu la Ulaya (Esa) linasema sehemu kubwa ya satelaiti hiyo ya tani mbili itaungua ikishuka.

Inawezekana baadhi ya sehemu zake zenye nguvu zaidi zinaweza kuhimili joto kali wakati inaposhuka kwa kasi ya juu, lakini uwezekano wa vipande hivi kuanguka maeneo yenye watu wengi na kusababisha uharibifu ni mdogo.

Vipande vyake vinaweza kutua popote duniani lakini kwasababu sehemu kubwa ya dunia imefunikwa na bahari, uchafu wowote una uwezekano mkubwa wa kuanguka baharini.

Share: