'Ubongo Bandia' wenye uwezo kuamsha tena Viungo au Uwezo wa Binadamu kufanya kazi ikiwemo kurejesha uwezo wa kuona na kutembea
Marekani: Kampuni ya Neuralink inayomilikiwa na Bilionea wa Dunia, Elon Musk inatafuta Mtu wa kumpandikiza Kifaa maalumu 'Ubongo Bandia' wenye uwezo kuamsha tena Viungo au Uwezo wa Binadamu kufanya kazi ikiwemo kurejesha uwezo wa kuona na kutembea kwa waliopata tatizo la Kiharusi
Awali, Neuralink ilikuwa na matumaini ya kupata kibali cha kupandikiza 'BrainChip' kwa Wagonjwa 10, lakini Mamlaka ya Chakula na Dawa (FDA) ilipunguza idadi baada ya kuibua wasiwasi kuhusu Usalama kwa Binadamu
Taarifa zinaeleza upandikizaji unahusisha kufunguliwa Fuvu la Kichwa na kuunganishwa 'Kiolesura' cha Kompyuta (Brain-computer interfaces) kinachofanya kazi sawa au zaidi ya Ubongo. Hata hivyo katika majaribio ya awali Wanyama 1,500 walifariki.