Lengo la kampuni ni kuunganisha akili za binadamu na kompyuta ili kusaidia kukabiliana na changamano za neva.
Bilionea wa teknolojia Elon Musk amesema kwa mara ya kwanza kampuni yake ya Neuralink imefanikiwa kupandikiza kifaa maalum cha eletroniki kwenye Ubongo wa binadamu kisichotumia nyaya.
"Binadamu wa kwanza kuwekewa kipandikizi kutoka Neuralink anaendelea vizuri". - Elon Musk
Lengo la kampuni ni kuunganisha akili za binadamu na kompyuta ili kusaidia kukabiliana na changamano za neva.
Inatarajiwa kuwa kifaa hicho kuwa kiunganishi cha ubongo na kitawasaidia watu waliopooza viungo kuweza kudhibiti vifaa kama simu na kompyuta wakitumia fikra zao.
Katika chapisho lake kwenye X, zamani Twitter, Musk alisema kwamba mgonjwa "anaendelea vizuri," na kwamba matokeo ya awali yanaonesha matumaini.