Chuo cha tehama kujengwa jijini la dodoma nala

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeanza utekelezaji wa ujenzi wa Chuo Mahiri cha TEHAMA katika Jiji la Dodoma eneo la Nala .

Utekelezaji wa Miradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa tatu wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2021/2026 na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020/2025 ambayo inasisitiza uwepo wa mafunzo ya Ujuzi na Ubunifu katika TEHAMA nchini.

Hayo yamebainishwa na Katibu Makuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla leo Januari 29 Jijini Dodoma katika mkutano na Wanahabari wakati wa kikao cha ufunguzi wa ujenzi wa Chuo Mahiri cha TEHAMA Dodoma kati ya Wizara hiyo na Washauri Elekezi Chuo cha Hanyang kutoka nchini Korea. 

Katibu Mkuu huyo amasema Vyuo hivyo vya TEHAMA vitakua kitovu cha taaluma, Ujuzi, ubunifu, Tafiti, Maarifa na kukuza ujasiri amali wa kidijitali Kitaifa na Kimataifa.

Ujenzi wa Chuo hicho cha TEHAMA utachochea maendeleo katika wakati huu wa Mapinduzi ya 4, 5 na 6 ya viwanda ambayo ndio chachu ya ukuaji wa Uchumi wa Kidigitali Duniani.

Pia ,Chuo hicho kitaifanya Tanzania kuwa mahali pazuri na kuvutia Utalii wa Kidijitali,

Kujifunzia, na kuongeza uwekezaji kutokana na upatikanaji endelevu wa jamii yenye Maarifa yanayoendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia Duniani.

Share: