Bunge la seneti lameidhinisha mswada unaoweza kusababisha tiktok kupigwa marufuku nchini marekani.

Bunge la Seneti lameidhinisha mswada wa kihistoria wenye utata ambao unaweza kusababisha TikTok kupigwa marufuku nchini Marekani.

Mswada huo unampa mmiliki wa TikTok Mchina, ByteDance, miezi tisa kuuza hisa zake au programu itazuiwa Marekani.

Mswada huo sasa utakabidhiwa Rais wa Marekani Joe Biden ambaye, amesema atautia saini kuwa sheria punde utakapofika kwenye meza yake.

Iwapo hilo litatokea, ByteDance italazimika kutafuta idhini kutoka kwa maafisa wa China ili kukamilisha mauzo ya kulazimishwa, ambayo Beijing imeapa kupinga.

Hata hivyo, wachambuzi wanasema mchakato huo unaweza kuchukua miaka.

Mtendaji mkuu wa TikTok, Shou Zi Chew, alisema mwezi uliopita kampuni itaendelea kufanya yote iwezayo ikiwa ni pamoja na kutumia "haki zake za kisheria" kulinda jukwaa.







Share: