Arion Kurtaj Awekwa kizuizini baada ya kudukua video game ya gta vi

Mdukuzi aliyejulikana kwa jina Arion Kurtaj, mwenye umri wa miaka 18, mkazi wa Oxford nchini Uingereza, ambaye alihusishwa na udukuzi wa program ya michezo ya video (Video Game) ya Grand Theft Auto VI, inayotarajiwa kutoka mnamo 2025, amehukumiwa kifungo cha muda usiojulikana ndani ya hospitali, hadi pale madaktari watakapoithibitishia mahakama kuwa kijana huyo si hatari tena kwa umma.

Kurtaj ambaye aliwahi kuwa mfuasi wa genge la kimataifa la udukuzi linalojulikana kama Lapsus$, anakabiliwa na hali ya usonji(Autism) na alibainika kuwa alifanya mashambulizi ya kimtandao dhidi ya kampuni ya Rockstar Games, ambao ndio watengenezaji wa GTA VI.

Kulingana na BBC, imeelezwa kuwa Kijana huyo, licha ya kunyang'anywa kompyutampakato(laptop), alipokuwa nje kwa dhamana baada ya kudukua kampuni ya Nvidia, ambapo aliwekwa hotelini chini ya ulinzi wa Polisi lakini bado alifanikiwa kuishambulia kampuni ya Rockstar Games kisha kuiba na kuvujisha video 90 za GTA VI, kwa kutumia Runinga(TV), Amazon Fire Stick ya chumba hicho pamoja na simu janja, keybord na kipanya cha kompyuta (Mouse).

Mahakama hiyo ilielezwa kuwa Kurtaj, alifanya vurugu alipokuwa kizuizini na kusababisha uharibifu wa mali na kwamba alionyesha dhamira yake ya kurudi kwenye uhalifu wa mtandaoni haraka iwezekanavyo. 

Share: