Afrika kusini imezindua teksi za kidijitali maalumu kwa wanawake kwa nia ya kuwalinda dhidi ya uhalifu.

ongezeko la uhalifu hasa matukio yanayohusisha wanawake ambao wamekuwa waathirika wakati wa kutumia teksi

Kgosigadi Rides, ikiwa na maana ya safari za malkia, iliyozinduliwa na kikundi cha wanawake wa Afrika Kusini, inaunganisha madereva wa kike na abiria wa kike, ili kufanikisha usafiri salama na wa kuaminika pamoja na kutatua masuala ya usalama yanayowakumba wanawake na wasichana nyakati zote.

Afrika Kusini imeshuhudia ongezeko la uhalifu, hasa matukio yanayohusisha wanawake ambao wamekuwa waathirika wakati wa kutumia teksi zinazoendeshwa na wanaume.

Share: