Waziri mkuu ampongeza dkt. tulia kwa ushindi wa urais

Ninaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kukupongeza kwa dhati ya moyo wangu Dkt. Tulia Ackson, Mbunge wa Mbeya Mjini na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuaminiwa na kuchaguliwa kuwa Rais wa 31 wa Umoja wa Mabunge ya Dunia (IPU).

Ushindi huu ni kielelezo cha imani kubwa ambayo Mataifa mengi Duniani wanayo juu ya nchi yetu na wewe mwenyewe.

Ninakutakia kheri katika jukumu hili linalounganisha Mataifa yetu pamoja ili kujadili mwelekeo chanya wa Dunia.

Hongera sana kwa ushindi.




Share: