
Kwa mujibu wa Katibu wa CCM Wilaya ya Kongwa, Joyce Mkaugala ,Kufuatia kifo cha aliyeongoza kura za maoni Jimbo la Kongwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)...
Job Ndugai ametangaza upya mchakato wa kuchukua fomu utafanyika kwa siku moja ambayo ni leo Jumanne Agosti 12, 2025 na kura hizo sasa zitapigwa upya Jumapili Agosti 17, 2025.
Mkaugala amesema na kura zitapigwa leo kwa utaratibu wa wajumbe ngazi ya kata kama ilivyofanyika Agosti 4, 2025 na baadaye vikao vya kawaida vitaendelea.
"Ni kweli tunatoa fomu kwa siku moja ya leo (Agosti 12,2025) baada ya hapa tunaendelea na taratibu za kawaida ambapo Jumapili ya terehe 17,2025 wajumbe watapiga kura za maoni," amesema Mkaugala.
Share: