MAANDALIZI YAMEPAMBA MOTO TUME HURU YA UCHAGUZI KWELEKE OCTOBA 2025

Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) inaendelea na maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025 kwa kutoa mafunzo kwa watendaji na wasimamizi wa uchaguzi kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Mafunzo hayo, yanayoendelea leo Julai 22 jijini Dar es Salaam, yalianza rasmi Julai 21 na yanatarajiwa kuhitimishwa Julai 23, 2025 lengo kuu likiwa ni kuwajengea uwezo washiriki katika kutekeleza majukumu yao ya kikatiba kwa kuzingatia sheria, taratibu, na kanuni za uchaguzi.


Katika mafunzo hayo, mada mbalimbali zimewasilishwa kwa njia ya nadharia na vitendo, zikiongozwa na maafisa wa INEC wenye uzoefu na ujuzi wa masuala ya uchaguzi.


Aidha, washiriki wamepata fursa ya kujifunza mbinu bora za usimamizi wa uchaguzi, usimamizi wa vituo vya kupigia kura, pamoja na matumizi sahihi ya vifaa vya uchaguzi.

Share: