Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI Mhe. Mohammed Mchengerwa leo Novemba 27, 2024, amekuwa miongoni mwa Watanzania walioitumia vyema haki yao ya msingi na ya kikatiba ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa watakao waongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.