Waziri Mchengerwa akemea mivutano baina ya viongozi

Akimnukuu Hayati Nelson Mandela, Rais wa zamani wa Afrika kusini aliyewahi kusema kuwa Uongozi mzuri unahusisha kuwajibika kwa heshima na uaminifu, Mhe. Mchengerwa amesisitiza kuheshimiana na kushirikiana kwa Viongozi ili kuhakikisha wanakuwa na mchango katika maendeleo ya Tanzania na watu wake.

"Tunatambua zipo changamoto ambazo zinaweza kuibuka katika maeneo yetu, lakini msingi wa Taifa letu na Baba wa Taifa alituhusia ni Umoja na Mshikamano, Viongozi wa kuteuliwa na kuchaguliwa tunapovutana wenyewe kwa wenyewe lazima tutambue kuwa matamanio ya Taifa letu hayataweza kufikiwa kwa mivutano kati yetu. Tuheshimiane kila mmoja kwenye nafasi na kuheshimiana." Amesema Mhe. Mchengerwa.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mchengerwa akirejea sintofahamu iliyotokea Simanjiro Mkoani Manyara, amewapongeza Wakuu wa Mikoa, wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali nchini kwa kazi nzuri wanayoifanya akiwataka kuendelea kuwa chachu ya maendeleo kwenye maeneo yao ya kazi.

Share: