Kamanda wa Polisi Mkoa, Philemon Makungu amesema “Sio ACT tu waliokamatwa hata wa CCM tuliwashikilia, walifanya fujo, upelelezi unaendelea ukikamilika watafikishwa Mahakamani
Viongozi kadhaa wa Chama cha ACT Wazalendo akiwemo Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa, Abdul Nondo wanatarajiwa kupandishwa Mahakamani muda wowote kuanzia Machi 27, 2024 wakidaiwa kufanya fujo dhidi ya Mwanachama wa CCM waliyedai ana kura bandia, Kata ya Kasingirima, Jimbo la Kigoma Mjini (Machi 20, 2024)
Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa ACT, Shangwe Ayo amesema watuhumiwa wengine ni Alumbula Khalidi, Alhaji Selemani Simba, Ntakije Ntanena na Khamis Mzungu
Kamanda wa Polisi Mkoa, Philemon Makungu amesema “Sio ACT tu waliokamatwa hata wa CCM tuliwashikilia, walifanya fujo, upelelezi unaendelea ukikamilika watafikishwa Mahakamani.”
Aidha, Nondo amesema “Licha ya kufunguliwa Mashtaka, mimi pia nilifungua jalada la kesi kwa OCCID dhidi ya Polisi Kituo cha Kati aliyetumia "Unreasonable Force" dhidi yangu kwa kunipiga kinyume na PGO kifungu cha 15 na 16.”