Uchaguzi mkoa wa Iringa unaendelea vizuri na Hali iko shwari , RC Serukamba

Mapema leo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba ameshiriki katika zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika leo Novemba, 27, 2024 nchini kote.


Akizungumza mara baada ya kupiga kura Serukamba amesema kuwa hali ya Usalama kwa Mkoa wa Iringa ni shwari kabisa na matarajio yao ni kuona hali hii ya utulivu na usalama inakwenda vyema mpaka mwisho wa zoezi hili. 


"Uchaguzi wetu umeenda vizuri toka umeanza saa mbili asuubuhi sijasikia tatizo lolote kwa maana ya Mkoa mzima wa Iringa, Uchaguzi umekuwa wa huru na wa haki na sisi Watu wa Mkoa wa Iringa tumedhamiria kufanya Uchaguzi wa huru na haki" amesema Serukamba 


Kwa upande wao baadhi ya Wapiga kura katika Vituo tofauti tofauti Manispaa ya Iringa wamesema kuwa Uchaguzi umeenda Vizuri na Unaendelea vizuri huku wakiiomba Serikali kuendelea kuhakikisha ulinzi na usalama mpaka mwisho mwa zoezi hili.


Shiriki kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa na uwe sehemu ya maamuzi ya mtaa/Kijiji chako kwa maendeleo ya ustawi wa eneo lako.

cc @ortamisemi @mohamed_mchengerwa

#MitaaInaamua

#Novemba27

#novembayamitaa

Share: