Tupige kura kumshukuru rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka WanaCCM Bukombe kujitokeza kupiga kura ya kuwachagua viongozi wao katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kama shukrani kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa miradi mingi ya maendeleo iliyotekelezwa Wilaya ya Bukombe na Serikali ya awamu ya sita.



Dkt. Biteko amesema hayo Novemba 21, 2024 katika Kata ya Igulwa, Bukombe mkoani Geita wakati akizindua Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 Mwaka huu. "Jitokezeni kupiga kura ili kumlipa Dkt. Samia kwa upendo kufuatia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya elimu, umeme, barabara, taa za barabarani, maji na vituo vya afya,” amesema Dkt. Biteko

Amewataka watu wa Bukombe kuwachagua Viongozi wenye uwezo wa kuwasemea na kuleta maendeleo kwa ujumla. “huku akisisitiza kwa Wanabukombe kukamilisha kazi waliyonayo tarehe 27/11/2024 ambayo ni moja tu ya "kubeba vyote,”akimaanisha ushindi wa CCM kwa nafasi zote zinazogombewa. Ameongeza “ Tumefanya kazi kubwa kwenye uandikishaji, hatuna budi kujisifu ingawa haipendezi, Mmetuheshimisha na matokeo mtayaona,”



Amewahimiza wagombea watakapochaguliwa kuhudumia wananchi bila ubaguzi wa kabila wala itikadi pamoja na changamoto ambazo wanaweza kukabiliana nazo ili kuleta maendeleo kwa wananchi.Naye, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukombe Daniel Rutonja amesema asilimia 52 ya wagombea katika ngazi ya vijiji walipita bila kupingwa na asilimia 70 katika ngazi ya vitongoji hawakupata upinzani.

Kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchi nzima zimeanza rasmi tarehe 20 Novemba, 2024 na zitahitimishwa tarehe 26 Novemba 2024 ambapo vyama mbalimbali vinatarajia kushiriki uchaguzi huo ambao siku ya tarehe 27/11/2024 itakuwa ni siku ya kupiga kura.


#STBongoUPDATES #NyumbaniKwanza

Share: