Tume ya taifa ya uchaguzi ya rwanda (nec) imeondoa jina la diane rwigara mpinzani wa rais paul kagame

Ikumbukwe, Rais Paul Kagame ametawala Rwanda tangu mwaka 1994 kwa kivuli cha Makamu wa Rais na kuwa Rais kamili mwaka 2003

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Rwanda (NEC) imeondoa jina la Diane Rwigara, mpinzani wa Rais Paul Kagame katika orodha ya Wagombea Urais unaotarajiwa kufanyika July 14, 2024

Mwenyekiti wa NEC, Oda Gasinzigwa amesema Rwigara alishindwa kuwasilisha baadhi ya nyaraka zilizohitajika kumthibitisha katika nafasi ya Ugombea, zikiwemo Taarifa za Kumbukumbu za Uhalifu na Saini za Wajumbe, zoezi ambalo limeshafungwa tangu Mei 30

Mwaka 2017, Diane Rwigara aliondolewa pia katika mchakato wa kuwania Urais kwa madai ya kukosa Vigezo huku familia yake ikiripotiwa kukumbana na matatizo mfululizo yakiwemo ya vifo vya Wanafamilia na kutaifishwa kwa baadhi ya biashara zao

Ikumbukwe, Rais Paul Kagame ametawala Rwanda tangu mwaka 1994 kwa kivuli cha Makamu wa Rais na kuwa Rais kamili mwaka 2003

Share: