Takriban robo tatu ya Wamarekani wanaishi katika majimbo ambako bangi ni halali kutumiwa kwa ajili ya matibabu. Nusu ya idadi ya watu wanaishi katika maeneo ambako bangi inaruhusiwa kwa starehe.
Bangi ni suala nadra la makubaliano katika Amerika iliyogawanyika kisiasa, huku ukusanyaji maoni ukionyesha kwamba asilimia 88 ya Wamarekani wanaunga mkono walau kwa kiasi fulani kuhalalisha bangi.
Lakini watetezi wa zao hilo wanasema hakuna mgombea hata mmoja wa juu wa urais anatumia mitazamo inayobadilika.
Takriban robo tatu ya Wamarekani wanaishi katika majimbo ambako bangi ni halali kutumiwa kwa ajili ya matibabu. Nusu ya idadi ya watu wanaishi katika maeneo ambako bangi inaruhusiwa kwa starehe.
Lakini Bangi bado inaendelea kutizamwa kuwa si halali kwa mujibu wa sheria ya serikali kuu, ambako imewekwa pamoja na heroine na LSD kama dawa isiyo ya matumizi ya matibabu yanayokubalika kwa hivi sasa na kuna uwezekano mkubwa ikatumiwa vibaya.
Idadi kubwa ya wapiga kura wa Marekani ambao wanadhani kwamba ni vyema mabadiliko yafanyike kwa bangi ni fursa muafaka kwa wagombea urais Joe Biden na Donald Trump, hasa miongoni mwa wapiga kura vijana, kwa mujibu Scotty Smart, ambaye ni mratibu wa jumuiya katika kundi la kiraia la New Georgia Project.
Scotty Smart, New Georgia Project anaeleza: “Watu wengi hawaelewi sera. Watu wengi hawafahamu jinsi sera zinavyoathiri maisha ya kila siku. Nadhani zao la bangi ni suala ambalo linachochea na kuwasisimua vijana wadogo kulipa mtizamo.”
Caroline Phillips, National Cannabis Festival amesema: “Kwa wote hao, jambo moja ambalo wanafana ni kwamba rekodi yao juu ya bangi imekuwa haiendani na inaongezeka. Tumesikia ahadi kutoka kwa tawala zote mbili, hakuna hata moja ambaye amejitokeza wazi wazi.”