Serikali Kuanzisha Baraza la Afya ya Akili

Serikali inatarajia kuanzisha Baraza la afya ya akili nnchini litakalosimamia muundo utakaoratibu sekta mbalimbali za kitaaluma na kiutendaji ili kushugulikia ufanisi wa suala la afya ya akili.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo 31 October, 2024 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mhe. Jesca Msambatavangu aliyetaka kujua tamko la serikali kuhusu kuanzisha Baraza hilo baada ya kukithiri matukio yasiyo ya kawaida yanayochangiwa na tatizo la afya ya akili ikiwemo wizi, mauaji na mapenzi ya jinsia moja.

Share: