Rc chalamila atoa mkono wa sikukuu kwa viongozi ccm-dsm

RC Chalamila akiongea na viongozi hao ametumia nafasi hiyo kujitambulisha rasmi katika chama hicho ikiwa ni mara ya kwanza kukutana na viongozi hao kwa wingi toka apangiwe na Mhe Rais kuhudumu katika Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Desemba 21, 2023 ametoa mkono wa Sikukuu kwa viongozi CCM kuanzia ngazi ya Mkoa, Wilaya,Kata na Mitaa wakati wa mkutano maalum wa viongozi hao ambao uliongozwa na mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Mhe Abbas Mtevu katika Ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni.

RC Chalamila akiongea na viongozi hao ametumia nafasi hiyo kujitambulisha rasmi katika chama hicho ikiwa ni mara ya kwanza kukutana na viongozi hao kwa wingi toka apangiwe na Mhe Rais kuhudumu katika Mkoa huo.

RC Chalamila amesema toka aanze kuhudumu katika Mkoa huo amepata na anaendelea kupata heshima kubwa na kuungwa mkono sana na CCM " Nimekuja Dar kwa kuhamishiwa nikitoka Mkoa wa Kagera nipende kutumia fursa hii kumshukuru sana Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini" Alisema RC Chalamila

Aidha RC Chalamila amesema kila mwanachama wa CCM ni vizuri kuneneana vema kwa masilahi mapana ya chama, lazima tuwe imara katika kukabiliana na chokochoko hususani nyakati hizi za kuelekea kwenye uchaguzi."Nitasimama imara usiku na mchana na CCM, imani yangu katika Siasa ni CCM, na sitamuonea mtu aliyoko nje ya CCM" Alisisitiza Chalamila.

Vilevile ametoa rai kuendelea kumuunga mkono mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Samia Suluhu Hassan na kila mmoja kuwa washauri wazuri wa Amani pia kutoa elimu ya uchaguzi kwa kuhakikisha chama kinateua watu wazuri wanaopendwa na watu wengi katika maeneo yao.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama Mkoa Mhe Abbas Mtevu Akifungua Mkutano huo amewataka viongozi katika maeneo yao kujipanga na ushindi wa kishindo katika mitaa yote na sio kwa goli la mkono, "Kata ikipoteza mtaa sitakuwa pamoja na kiongozi husika uliomba nafasi mwenyewe ya uongozi kafanye kazi", pia amewataka Wakuu wa Wilaya kuweka mzingira wezeshi ya kiuchumi kwa watu kwa kufanya matamasha yanayoibua fursa kwa watu kama ilivyofanyika kwa Wilaya ya Kigamboni.

Share: