Rc albert chalamila: ccm pamoja na vyama vingine vyote hatupaswi kuhitilafiana kwa itikadi za vyama vyetu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila akiwa anaendelea na usafi katika eneo la Mbezi Jijini Dar es salaam amekutana na baadhi ya Watu wakiwa wanashiriki maandamano ambapo ameongea nao na kuwataka waendelee kuandamana ili kufikisha ujumbe wao panapostahili huku akiwasihi maandamano hayo yalinde uwekezaji uliofanywa Dar es salaam.

Chalamila amesema “Dar es salaam ndipo vinakotoka viwanda vingi, ndipo pana Hospitali kubwa, mzunguko mkubwa wa fedha na uwekezaji mkubwa kwahiyo maandamano yetu yanapaswa kulinda huo uwekezaji ambao Nchi imeshafanya kwasababu Mtoto wako wewe na Mtoto wangu tutafaidika na huo uwekezaji kwa pamoja, tukipaharibu Dar es salaam hatuna mahali pa kukimbilia”

“Kwahiyo Mh. Rais pamoja na Viongozi wote wamesema acha Watu waandamane wakifikishe ujumbe wao panapostahili, huku pia tukiamini kwamba CHADEMA kama Chama kikubwa katika Nchi yetu, CCM pamoja na Vyama vingine vyote hatupaswi kuhitilafiana kwa itikadi za Vyama vyetu”

“Mimi RC wenu naendelea kufanya usafi na kwasababu sasa hivi kuna mlipuko mkubwa wa magonjwa tunaendelea kufanya usafi na nyinyi endeleeni kufikisha ujumbe kwa Jamii mliyoikusudia”

Share: