Rais wa afrika kusini cyril ramaphosa amekikosoa chama kikuu cha upinzani nchini humo

Barua ya DA kwa serikali ya Marekani bila shaka inakaribia kujaribu kuuza nchi yetu kwa mamlaka nyingine duniani

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amekikosoa chama kikuu cha upinzani nchini humo, Democratic Alliance (DA) kwa kuomba waangalizi wa Marekani na nchi za Ulaya kufuatilia uchaguzi ujao.

Chama hicho kilitoa ombi hilo katika barua iliyotumwa wiki iliyopita kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na baadhi ya mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya

"Barua ya DA kwa serikali ya Marekani bila shaka inakaribia kujaribu kuuza nchi yetu kwa mamlaka nyingine duniani," Rais Ramaphosa alinukuliwa na shirika la utangazaji la SABC akisema.

"Na tuna mashirika ya kikanda duniani kama Sadc, AU na tuna UN pia. Wanakuja kufuatilia chaguzi zetu na sasa kwa taasisi isiyo ya serikali kuuza demokrasia yetu."

Chama tawala cha African National Congress (ANC) pia kiliikashifu DA kwa barua hiyo siku ya Jumamosi, kikishutumu chama cha upinzani kwa kunadi "uhuru wa Afrika".

Uchaguzi wa Afrika Kusini umepangwa kufanyika tarehe 29 Mei.

Kura za maoni za makampuni ya utafiti zinaonyesha kuwa sehemu ya ANC ya kura inaweza kushuka chini ya 50% kwa mara ya kwanza tangu ilipoingia madarakani mwaka 1994, ikichochewa na kuenea kwa kutoridhika na hali ya uchumi, huduma za umma na rushwa.




Share: