Rais samia : miaka 60 tumeshirikiana ujerumani na tanzania

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Ujerumani Dkt. Frank Walter Steinmeier wameongea na Waandishi wa Habari Ikulu Dar es salam leo October 31,2023 ambapo pamoja na mambo mengine Rais Samia amesema Ujerumani na Tanzania ni Marafiki ambao wameshirikiana kwenye mambo mengi kwenye uhusiano ambao umefika miaka 60 sasa.

Rais Samia amesema “Nchi yetu imepiga hatua nyingine ya kihistoria katika uhusino wake na Ujerumani, tumemkaribisha Rais wa Ujerumani hapa nchini, nakushukuru sana Mh.Rais kwa kukubali ziara ya kuitembelea Tanzania, ni heshima kwangu kukukaribisha wewe na ujumbe wako hapa Ikulu, karibuni sana”

“Leo asubuhi Mimi na Rais wa Ujerumani tumezungumza masuala mengi muhimu kuhusu uhusiano na ushirikiano wa Nchi zetu lakini hapa nitagusia baadhi, uhusiano wetu umefika miaka 60 sasa na katika kipindi chote hicho tumekuwa tukishirikiana vema, Serikali ya Ujerumani imekuwa rafiki ambayo tumeshikana nayo mkono kwenye masuala mengi”

“Suala la Bima ya Afya tulitaka usaidizi kwao watusaidie, Serikali ya Ujerumani inajenga Hospitali kubwa ya Jeshi pale Dodoma lakini pia tuliomba watusaidie kujenga Hospitali kubwa ya kisasa ya maradhi ya kuambukiza pale Lugalo, wanatusaidia kwenye maji, elimu upande wa scholarship, elimu ufundi, utamaduni, michezo, Ulinzi n.k, katika mazungumzo yetu tumesisitiza umuhimu wa kukuza ushirikiano huu”

“Katika hili tumezielekeza Timu za Wataalamu wa Tanzania na Ujerumani kuendelea na mazungumzo ya mara kwa mara kuboresha maeneo ya ushirikiano, nimemuhakikisha Mh.Rais kwamba Serikali ya Tanzania ipo tayari kuwa Mwenyeji wa mazungumzo yajayo ya ushirikiano yatakayofanyika mwakani

Share: