Rais samia ampongeza dkt. tulia kwa ushindi

Rais Samia atoa salamu za Pongezi kwa Spika Dt. Tulia kwa Ushindi wa Urais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU)

Rais Samia ameandika kuwa : Pongezi za dhati kwa Spika wa Bunge letu, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU). Ushindi huu ni ushuhuda wa kazi kubwa unayoendelea kuifanya na imani wajumbe waliyo nayo juu yako na nchi yetu. Kuchaguliwa kwako pia ni matokeo ya miaka mingi ya kazi, weledi na kujituma katika utumishi wa umma, mfano bora kwa watoto wa kike katika nchi yetu, Afrika na hata nje ya mipaka ya bara letu

Share: