PICHA 20 : SHANGWE NA MATUKIO ,CCM MKUTANO MKUU DODOMA 2025

Hapatoshi makao makuu ya CCM,Jiji la dodoma limetaradadi na uwepo wa viongozi,wajumbe, wageni waalikwa ,wanachama na wengine kibao , tukiwa tunaelekea uchaguzi mkuu wa Raisi na viongozi wengine wa nafasi za juu katika serekali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkutano huo unatajiwa kuwa na ajenda tatu ikiwamo ya uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi wa chama hicho 2025/2030.



Pia, wajumbe watakuwa na kazi ya kupokea na kujadili utekelezaji wa Ilani za uchaguzi ya mwaka 2020 hadi 2025 wa serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Ajenda nyingine katika mkutano ni mabadiliko madogo ya Katiba ya chama hicho.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Matukio tofautitofauti ya Picha aliposhiriki Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Taifa wa mwaka 2025 uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete JKCC Mkoani Dodoma leo Mei 29,2025.


Mkutano huo umetanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani humo Mei 27 kikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan.

Kkao hicho kilifuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kitachofanyika Dodoma Mei 28 katika Ukumbi wa NEC uliopo kwenye jengo la White House jijini Dodoma.




Januari 18, mwaka huu CCM ilifanya Mkutano Mkuu wa CCM jijini Dodoma na wajumbe waliwapitisha kwa kauli moja Rais Samia kuipeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.


Pia, mkutano huo ulimpitisha Katibu Mkuu wa chama hicho, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi awe mgombea

mwenza wa CCM na Stephen Wassira kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara akichukua

nafasi ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Abdulrahman Kinana aliyeng’atuka nafasi hiyo.


Kupata taarifa na picha kuhusu  kinachojiri , Endelea kutembelea tovuti ,na mitandao yetu ya kijamii instagram na facebook @Stbongotv pia Ungana nasi kupitia kisumbuzi @startimestz CH 161 (antena) CH 401 (Dish) pamoja na kwenye YouTube channel yetu ya #STBongoTV Kwa Taarifa zaidi.


#STBongoUpdates #NyumbaniKwanza

Share: