Paul makonda: tuna kila sababu ya kutembea kifua mbele kwa kazi nzuri na heshima anayoipa chama chetu dkt samia suluhu hassan

Nimekuja kutazama utekelezaji wa ilani. Na hakika ni kwamba Rais wetu anapotimiza miaka mitatu ya uongozi ambaye pia ndiye mwenyekiti wetu wa chama, tuna kila sababu ya kutembea kifua mbele kwa kazi nzuri na heshima anayoipa chama chetu na nchi yetu kwa uaminifu wake na uzalendo wake kwa taifa letu.

Kuna kasumba ya ujinga unaoendelea wa kutaka kumtofautisha Daktari Samia Suluhu Hassan na Dkt John Pombe Magufuli.

"Huwezi kuwatenganisha hawa watu, na viongozi wengi wanafiki wanaotafuta kujipendekeza kwa Dkt Samia kila wakipata jukwaa wanataka kumfanya kama Dkt. Samia sio sehemu ya Dkt. Magufuli.

Kama msemaji wa chama, chama ambacho tulizunguka na ilani ya chama chetu, kila anachokifanya Dkt. Samia ndicho ambacho alikifanya Dkt. Magufuli.

Na watu hawa walisimama wakazunguka katika taifa hili wakatafuta kura kwa pamoja, huwezi kuwatenganisha, na waziri mkuu wao ni Kassim Majaliwa.

Natamani leo iwe ni siku ya mwisho ya unafiki wa viongozi na wanasiasa uchwara wanaopambana kuwatenganisha viongozi hawa. Mafanikio haya tunayasherehea wote kwasababu chama ni kimoja, serikali ni ya CCM na ninyi wananchi mlitupigia kura."

Paul Makonda

Katibu wa NEC itikadi, uenezi na mafunzo wa ccm

Share: