Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi amesema uamuzi wa kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar ulizingatia kutanguliza mbele usalama wa maisha ya watu, maslahi, utulivu na mstakabali mwema wa Zanzibar, Wazanzibar na Watanzania wote kwa ujumla, kuliko vyama vya siasa.Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi amesema hayo alipokuwa akizungumza na Wazee wa Zanzibar
Balozi Dk. Nchimbi ameongeza kusema kuwa uwepo wa Serikali hiyo Zanzibar umeondoa hali ya siasa za chuki na uhasama mkubwa uliokuwepo kabla ya kufikiwa kwa uamuzi wa kuundwa kwake, huku akisisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kutimiza wajibu wake wa kutoa uongozi kwa nchi ili kudumisha umoja na utulivu uliokusudiwa kwa maslahi ya Wazanzibar na Watanzania wote.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi amesema hayo alipokuwa akizungumza na Wazee wa Zanzibar, Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, leo Jumapili, Machi 24, 2024, ikiwa ni siku ya pili akiwa kwenye ziara ya kikazi, akitokea Pemba, ambako pia alifanya mazungumzo na mashauriano na Wazee wa Pemba, Jumamosi, Machi 23, 2024.
Share: