Mwenezi makonda awasaidia kiasi cha fedha akina mama wenye ulemavu kujiendeleza kiuchumi

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amekutana na kuzungumza na akina mama wawili wenye ulemavu mara baada ya kumaliza kuzungumza na Wananchi wa Moshi Mjini kwenye Mkutano wa hadhara.

Ndugu Makonda aliwafata akina Mama hao waliokuwa na shauku ya kukaribiana nae wakionesha sura zenye furaha zenye tafsiri ya upendo uliojaa mioyoyoni mwao dhidi ya Chama Cha Mapinduzi kinachoongozwa na jemedali Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu. Samia Suluhu Hassan.

Mara baada ya kukutana na kuzungumza nao, walimueleza changamoto zao katika biashara zao wazifanyazo ambapo kwa Upendo wa CCM kwa Watanzania wote, Mwenezi Makonda alitoa kiasi kidogo cha fedha kuwakabidhi kwaajili ya kujiendeleza.

Makonda amewaambia akina mama hao ya kwamba shukrani zao ni waendelee kumuombea Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia kwani yeye ndiye aliyemtuma na anayafanya yote kwa niaba yake.

Share: