Mwenezi makonda atoa taarifa ya mrejesho wa semina ya mafunzo na kikao cha halmashauri kuu ya ccm taifa

Mwenezi Makonda ameeleza yaliyojiri katika Semina maalum ya Mafunzo kwa Wajumbe wa Halmshauri Kuu iliyofanyika siku ya tarehe 13 na 14 mwaka huu.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda akizungumza kwa kueleza yaliyojiri katika Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika mapema leo tarehe 15 Januari, 2024 Kisiwani Zanzibar kilochoendeshwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mwenezi Makonda ameeleza yaliyojiri katika Semina maalum ya Mafunzo kwa Wajumbe wa Halmshauri Kuu iliyofanyika siku ya tarehe 13 na 14 mwaka huu.

Katika Semina hiyo, Mwenezi Makonda amesema kuwa Wajumbe wamepata nafasi ya kushiriki kujua hatua zilizofikiwa katika Mradi wa Umeme wa Mwl. JK. Nyerere.

Pia, kujua hatua na kazi inayofanyika katika muendelezo wa Ujenzi wa Reli ya kisasa ya SGR.

Vilevile, kujua hatua na muendelezo wa utekelezaji wa Ujenzi wa Daraja la Magufuli (Kigongo - Busisi).

Pamoja na hayo, Wajumbe wamepata nafasi ya kujadili na kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 kwa upande wa Zanzibar.

Mwenezi Makonda amebainisha kuwa kupitia Kikao hicho, Wajumbe wampokea taarifa za maandalizi katika kuelekeza Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji 2024 na Maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za CCM kuelekea kufikisha miaka 47 mwezi februari mwaka huu.

Aidha, Mwenezi Makonda amesema Wajumbe wa Halmashauri Kuu kwa pamoja wamepokea jina kutoka kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa la atakayechukua kijiti cha nafasi ya Katibu Mkuu na kwa pamoja wameridhia kwa sauti moja ya kwamba Ndugu. Emmanuel John Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa.

Share: