Mshindani wa trump ajiondoa mbio za urais

Nikki Haley, mwanamama mshindani mkubwa wa Donald Trump kwenye kuwania nafasi ya kugombea Urais wa Marekani amejiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho na kusema "hajutii".

Kwa ukaribu zaidi kwa angalau wiki mbili sasa,Nikki na Trump walionekana kuchuana vikali ndani ya Republican licha ya Trump kumbwaga vibaya mwanamama huyo kwenye majimbo mengi ya Marekani.

Nikki amesema kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita alizindua kampeni yake ya urais akisema kampeni hiyo ilitokana na mapenzi makubwa kwa nchi yake hiyo.

Hata hivyo Nikki Haley hajatoa ridhaa yake kamili kwa rais huyo wa zamani bwana Donald Trump jambo ambalo wafuatiliaji wengi wa siasa walikuwa wakilisubiria kote ulimwenguni.

Share: