Mkenya ashinda uwakilishi jimbo la Minnesota Marekani

Momanyi, 39, anakuwa mwanasiasa wa kwanza mzaliwa wa Kenya kushikilia wadhifa wake nchini Marekani.

Momanyi alikuwa akigombea kiti hicho kupitia Chama cha Democratic-Farmer-Labor (DFL).

Alishinda asilimia 64.78 ya kura katika uchaguzi wa jana jumanne na kupata kiti katika kata ya 38A ya Minnesota, ambayo inajumuisha sehemu za kusini magharibi mwa Brooklyn Park na Osseo.

38A ni eneo lenye watu wa asili tofauti, na takriban asilimia 66 ya wakazi wanajitambulisha kama watu wa rangi, sehemu kubwa yao wakiwa wahamiaji Waafrika.

Momanyi alizaliwa katika Kaunti ya Nyamira, Kisii Magharibi mwa Kenya mwaka 1985 kwa wazazi na Tabitha na Philip Momanyi na alihamia Marekani pamoja na wazazi wake akiwa na umri wa miaka tisa na sasa ni mama wa watoto wawili.

Share: