Mbunge cherehani: ukiona kazi haina upinzani achana nayo,kazi yoyote ambayo ina maslahi kwa watu lazima iwe na upinzani.

Mbunge wa Ushetu mkoani Shinyanga Mhe.Emmanuel Cherehani amewasihi vijana kutokata tamaa pindi wanapoanza mapambano ya kuzifikia ndoto zao.

Mhe. Cherekani amesemaa hayo jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kikao cha baraza la umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi-UVCCM wilaya ya Kahama.

“Hapa kuna madaktari,kuna Wataalamu lakini mnakatishwa tamaa, na wengi mnaamua kurudi nyuma kinyonge … yupo mmoja mwenye maamuzi ambaye halali kila siku naye ni MUNGU….. ndiye anayejua ndoto za kila mtu aliyeko Duniani msiogope vijana wangu,”-Mhe Cherehani.

Share: