Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha demokrasia na maendeleo, (BAWACHA), Sharifa Suleiman ametangaza kuwa watafanya maadhimisho ya kitaifa ya siku ya wanawake jijini Dodoma.

Kiongozi huyo wa wanawake wa CHADEMA taifa kadhalika amewaambia wanahabari jijini Dar es salaam kuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Mh.Freeman Mbowe na wanatarajia kuwa na washiriki takribani 4,000 ambapo kauli mbiu ya siku hiyo ni 'Wekeza kwa Mwanamke kwa Maendeleo ya Taifa".

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hufanyika Machi 8 ya kila mwaka ili kusherehekea mafanikio ya wanawake na kujadili kuhusu vikwazo mbalimbali vinavyotatiza ustawi wao.

Share: