Matumizi ya kompyuta yazua changamoto katika upigaji kura drc

Baadhi ya wapiga kura Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wadai matumizi ya kompyuta katika uchaguzi yalikuwa kikwazo katika kufanikisha zoezi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano.

Baadhi ya wapiga kura waliiambia Sauti ya Amerika kuwa matumizi ya kompyuta yalisababisha changamoto kwa baadhi ya wapiga kura wengi wao wakisema hawajui na hawajawahi kutumia kompyuta tangu wazaliwe.

“Mashine imeharibika, hatujui kinachoendelea hapa” alisema mwanamke mmoja aliyejitokeza kupiga kura.

Wakati huo huo wakaazi wa baadhi ya mikoa wenye hasira wamezivunja kompyuta za Tume huru ya uchaguzi.

Share: