Makonda ataka wananchi kupewa kipaumbele.

Katibu wa NEC itikadi,uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Paul Makonda amesisitiza umuhimu wa ziara yake kwenye mikoa 20 ya Tanzania bara akisema inakisaidia Chama kufahamu changamoto mbalimbali za watendaji wa serikali na mifumo yake.

Mwenezi Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati alipopita kuwasalimia wananchi waliofika kwenye kliniki maalum ya kusikiliza kero za wananchi ikiwa ni utekelezaji wa agizo lake alilolitoa siku ya jana.

Mwenezi Makonda pia amesisitiza umuhimu wa kutumia lugha rafiki na ya kueleweka kwa wananchi wote ili kuwaridhisha wananchi wakati wa usikilizaji wa kero zao.

Share: