Profesa Chambo enzi za uhai wake alitumia zaidi ya miaka 30 kufundisha, kufanya tafiti mbalimbali na kutoa ushauri katika nyanja za uchumi, usimamizi wa ushirika, uchumi wa maendeleo na upangaji wa miradi mbalimbali.
Katibu wa NEC itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Ndugu Paul Makonda, leo amemtembelea nyumbani kwake mtaa wa Ushirika wa Neema mjini Moshi na kumjulia hali Bi. Gladys Chambo, mjane wa Profesa Suleiman Chambo.
Profesa Chambo alikuwa mhadhiri wa chuo cha Ushirika Moshi na akawa Mkuu na Profesa Mshiriki wa uchumi na usimamizi wa Asasi katika chuo cha Ushirika Moshi cha Chuo kikuu cha Ushirika na mafunzo ya biashara na miongoni mwa wanafunzi wake alikuwa Ndg. Paul Makonda.