Makonda afika ofisi za mkuu wa mkoa wa singida kufanya ukaguzi

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amefika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Singida kukagua agizo la Chama Cha Mapinduzi alilolitoa jana tarehe 25 kwenye Mkutano wa hadhara Mkoani Singida la kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Singida na Wakuu wake wa Wilaya kuanzisha Kliniki za kusikiliza kero mbalimbali na kuzitatua siku hiyohiyo kwa zile ambazo hazina mlolongo mrefu ilikusudi kuondoa maumivu yaliyo miyoyoni mwa Watanzania.

Mwenezi Makonda yupo mkoani Singida ambapo anatarajia kuelekea Mkoani Tabora kwa muendelezo wa ziara yake ya Mikoa 20 Back To Back.


Share: