Makamu mwenyekiti wa umoja wa vijana (uvccm) taifa, rehema sombi amewataka vijana kuwa watumiaji wazuri wa mitandao ya kijamii

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Rehema Sombi akiwa Mkoani Geita amewataka Vijana waendelee kuwa watumiaji wazuri wa mitandao ya kijamii haijalishi ni aina gani ya mtandao ya Kijamii wanayo tumia.

Sombi ametoa kauli hiyo wakati akifungua kambi la Vijana la Umoja huo katika kijiji cha Namonge Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, amesema kipekee matumizi ya Mitandao ya Kijamii yanayotokana na sayansi na teknolojia yamehuishwa kupitia mkataba baina ya chama na wananchi.

Amesema Vijana wajikite kuelezea mafanikio ya serikali zote mbili, vilevile kujinufaisha na fursa mbalimbali za kibiashara ili kujiingizia kipato na kwamba matumizi yakiwa kinyume chake yataleta athari kwa kizazi hiki na kizazi kijacho.

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Mohamed Kawaida aliomba serikali kufungia matumizi ya Mtandao wa X (TWITTER) kutokana na kuwa na maudhui yanayokwenda kinyume na maadili ya Kitanzania.

Share: