Makamu mwenyekiti wa (ccm) tanzania bara abdulurhaman kinana ameshiriki kikao maalumu cha halmashauri kuu ya ccm wilaya ya serengeti

Kinana amesema Viongozi wanapaswa kuendelea kuwaelimisha Wananchi kuheshimu mipaka iliyopo

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulurhaman Kinana amepokea malalamiko mbalimbali yakiwemo madai ya mauaji ya Wananchi katika Hifadhi ya Serengeti Mkoani Mara ambapo amesema hakuna mwenye haki ya kukatisha uhai wa Mtu mwingine.

Akiongea leo Mugumu, Serengeti Mkoani Mara, aliposhiriki kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Serengeti, Kinana amesema Viongozi wanapaswa kuendelea kuwaelimisha Wananchi kuheshimu mipaka iliyopo.

“Mkuu wa Wilaya ya Serengeti amelifafanua vizuri sana na huwezi kuulaumu upande mmoja peke yake lakini tunawajibu wa kuwaelimisha Wananchi kuhusu kuheshimu mipaka lakini jambo moja la msingi hakuna mwenye haki ya kuondoa uhai wa Mtu”.

Hata hivyo, amesema katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo tayari Serikali imeunda kamati ndogo ambayo itafika Mkoani Mara kufanya tathimini na hatimaye kutatua changamoto hiyo.

Share: