Mahakama ya kikatiba yatupilia mbali kesi zinazomhusu felix tshisekedi

Mahakama ya Kikatiba imetupilia mbali Kesi mbili zilizofunguliwa na baadhi ya Wagombea Urais nchini kongo waliopinga Mtaokeo ya Kura za Uchaguzi Mkuu uliompa Ushindi Felix Tshisekedi na hivyo kuidhinisha ushindi wake.

Mahakama hiyo imeidhinisha ushindi wa kiongozi huyo licha ya ripoti za Waangalizi Huru wakieleza kuwa Uchaguzi ulitawaliwa na dosari nyingi ikiwemo Vituo Kuchelewa Kufunguliwa, Wizi wa Kura na Udanganyifu kwenye baadhi ya Vituo.

Uamuzi huo unafungua njia kwa Tshisekedi kutumikia miaka mingine mitano kama mkuu wa nchi ya pili kwa ukubwa barani Afrika na mzalishaji mkuu wa Madini 'Cobalt' duniani pamoja na Madini mengine ya thamani kubwa kama Nickel, Almasi na Shaba.

Share: