Kinana awasili ruangwa

Akiwa wilayani humo kesho atakuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ruangwa

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amewasili wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikakazi ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Chama wa wilaya hiyo.

Kinana amewasili wilayani humo leo Januari 1, 2024 akiambatana na viongozi mbalimbali wa Chama wakiwemo baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Akiwa wilayani humo kesho atakuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ruangwa ambao pia utahudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa.

Share: