Kikao cha halmashauri kuu ya ccm taifa kufanyika jijini dar es salaam huku mrithi wa paul makonda akiteuliwa leo

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi anatarajiwa kuongoza kikao maalum cha Halmashauri kuu ya CCM Taifa kitakachofanyika leo jioni Jijini Dar Es salaam.

Kikao hicho kinafanyika wakati huu ambapo ndani ya Chama hicho kuna nafasi nne za wazi kwa wajumbe wa sekretarieti yake baada ya waliokuwa kwenye nafasi hizo kuteuliwa kwenye nyadhifa mbalimbali serikalini.

Nafasi hizo ni Naibu katibu mkuu bara,Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo, Katibu Mkuu wa umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi na Katibu Mkuu wa jumuiya ya wazazi wa chama hicho.

Ingawa nafasi zote hizo ni muhimu ndani ya Chama hicho kulingana na asili ya majukumu yake, macho na masikio ya wengi yapo kwenye kumjua mrithi wa Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo Bwana Paul Makonda aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha.

Share: