Kenya: kifungo cha miaka 5 jela kwa maafisa wa (iebc) watakaochelewesha kutangaza matokeo

Itakuwa ni makosa kwa Wajumbe na Wafanyakazi wa Tume ambao wanachelewesha kutangaza matokeo

Bunge limepokea Muswada wa Marekebisho ya Sheria za Makosa ya Uchaguzi wa Mwaka 2024 ambao unapendekeza kuwekwa Kifungo cha Miaka 5 jela kwa Maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) watakaochelewesha kutangaza Matokeo 

Muswada huo unasomeka "Itakuwa ni makosa kwa Wajumbe na Wafanyakazi wa Tume ambao wanachelewesha kutangaza matokeo ya Uchaguzi bila sababu au kwa makusudi au kubadilisha matokeo yaliyotangazwa.”

Aidha, imeelezwa kuwa Muswada huo unaoungwa Mkono na Vyama vyote, umependekeza makosa mapya ikiwa ni hatua ya kuongeza uadilifu ikiwemo kuruhusu upigaji kura wowote kufanywa katika vituo ambavyo havijatangazwa kwenye Gazeti la Serikali kuwa kinyume cha Sheria. 

Share: